Sherehe zetu za Makambi zinaanza rasmi leo jioni washiriki mnakumbushwa kukamilisha michango yenu na kuaandaa sadaka zetu za shukrani kwa Bwana, pia kuandaa mioyo kwa ajili ya kupokea Neno.
Kutakuwa na mikutano ya injili ya Rudi nyumbani itakayoanza tarehe 06 – 20/7/ 2024, Washiriki tujiandae.
Washiriki mnaendelea kukumbushwa kushiriki katika mpango wa Majengo wa tofali moja kwa kila Sabato. Hivi karibuni tunaanza kujenga ukuta wetu.
Kiongozi wa Uchapishaji anaendelea kuwaomba washiriki kuchangia na kununua vitabu.
Washiriki wote mnaombwa kujihusisha kuchangia na kununua vitabu vya Pambano Kuu na vingine na kuvisambaza
Vitabu vya kesha la asubuhi vimeshafika na vinapatikana kwa tsh 11500/=, watakaohitai waonane na Mzee Komaji.