Utusamehe Deni Zetu kama Nasi Tuwasamehevyo Wadeni Wetu

Fungu Elekezi: “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi” (Mt. 6:14).

“Sikuuhisi”

Alikuwa mzee na amekuwa mzee katika kanisa langu kwa miaka mingi. Kwa sasa alikuwa hospitalini. Nilipomtembelea, aliniambia, “Usiniombee, maana nimepotea.” “Kwa nini unasema hivyo?” nilimjibu. “Mchungaji, nimetenda dhambi. Nilifanya dhambi kubwa sana nilipokuwa kijana.” Je! Ulimwomba Mungu msamaha?” “Aa, naomba kila siku maishani mwangu, lakini kamwe hajanisamehe.” “Unawezaje kujua kuwa hajakusamehe?” “Naam,” alisema, sikuhisi kusamehewa.” Tuliongelea jambo hilo, mwisho wa mazungumzo yetu alikuwa na furaha na amani.

Unawezaje “kuuhisi” msamaha? Je! Ni hisia ya joto mwilini mwako au kitu cha baridi mikononi mwako, au mtekenyo nyuma ya shingo yako? Je! Unaweza kuunusa?

Biblia iko wazi. “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). Haisemi kuwa anasamehe dhambi ndogo tu au idadi fulani ya dhambi. Inasema wazi kwamba tukiziungama dhambi zetu, Hutusamehe ZOTE. Sharti ni kwamba: lazima utubu. Ahadi: Mungu anasamehe. Fanya sehemu yako na Mungu atafanya ya Kwake.

Msamaha si kitu ambacho unaweza kukihisi au kukithibitisha kisayansi. Ni kwa imani. Unalichukua Neno la Mungu kama lilivyo na kuamini kwamba Mungu hasemi uongo. Huwezi kuuelezea, hauustahili, lakini unajua kwamba Mungu aliahidi na ahadi Zake ni za hakika kwa asilimia

100 kwa sababu zinategemea tabia na Neno Lake. Hakuna kitu kilicho thabiti kuliko Neno la Mungu.

Unapoungama, mara moja unasamehewa. Yesu tayari alishalipa bei ya dhambi yako pale msalabani. Yeye ni “Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29). Damu Yake inatosha, na katika damu Yake mna ukombozi kwa ajili ya dhambi zenu zote (Efe. 1:7).

Baada ya kuungama unahitaji kuiweka Imani katika vitendo, ili kuchagua kuamini kwamba Mungu anafanya kile alichoahidi. “Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki” (Rum. 4:3). Kumbuka, “Mwenye haki ataishi kwa Imani” (Rum. 1:17). Unapoamini, Mungu anatenda, na unakuwa umesamehewa. Usijaribu kuuelezea au kudhani unaustahili. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu” (Efe. 2:8).

Kupitiajambohilirahisilakumwamini Mungu, Roho Mtakatifuamezalisha maisha mapya moyoni mwako. Wewe ni kama mtoto aliyezaliwa kwenye familia ya Mungu na Anakupenda kama vile ampendavyo Mwanawe” (Steps to Christ, uk. 52). Msamaha, haki, wokovu—vyote vinapokelewa kama zawadi kwa imani.

“Wewe ni mwenye dhambi. Hauwezi kulipia fidia kwa ajili ya dhambi zako zilizopita; hauwezi kuubadili moyo wako na kujifanya kuwa mtakatifu. Lakini Mungu anaahidi kufanya haya yote kwa ajili yako kupitia kwa Yesu. Wewe iamini tu ile ahadi…. Ukiiamini ahadi … Mungu anaweka ukweli…. Usingoje kuhisi kwamba umekamilishwa, bali sema, “ninaamini hivi, ndivyo ilivyo, si kwa sababu ninauhisi, bali kwa sababu Mungu ameahidi” (Steps to Christ, uk. 51).

Unapokaza macho yako kwenye msalaba wa Yesu, unapata taswira ya udhihirisho huo mkubwa wa upendo: Yesu, Mwumbaji, Yule anayetamka

na vinakuwa, Yule ambaye malaika hujifunika mbele Yake, Mungu wa Ulimwengu aliyeshuka na kuchukua umbo la mwanadamu. Yeye, Aliye Mtakatifu, alizichukua dhambi zako na kufa kwa ajili yako wewe binafsi. Mungu alikufa kwa ajili yako.

Kaza macho yako kwenye msalaba Wake. Kisha utagundua kwamba wale wanaopitia uzoefu wa neema pia huishiriki neema na wengine kwa ukarimu. Wale wanaopata msamaha, wanasamehe. Msingi wa msamaha wote unapatikana katika upendo wa Mungu tusioustahili, lakini kwa mtazamo wetu kwa wengine tunaonesha kama vile tumeufanya upendo huo kuwa wetu” (Christ’s Object Lessons, uk. 251).

Hebu Tuombe Pamoja

Muda wa Maombi (Dakika 30–45)

Vikundi vyote vya maombi vina njia tofauti za kuomba pamoja. Tunawahimiza kutumia dakika 30-45 zinazofuata katika maombi ya pamoja, kwa njia yo yote ambayo Roho Mtakatifu anaongoza. Tunahimiza maombi mafupi ya wazi (sentensi 1-3). Hii inaruhusu watu wengi zaidi kuomba mara nyingi. Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya kuomba kupitia Maandiko kulingana na mada. Unaweza kuomba kupitia vifungu vingine pia na kujumuisha masomo mengine katika wakati wako wa maombi. Tazama Mwongozo wa Kiongozi na Maombi ya Maombi ya Kanisa Ulimwenguni kwa mawazo ya maombi.

Kuomba Sawasawa na Neno la Mungu—Mathayo 6:14.

“Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.”

“Mkiwasamehe Watu Makosa Yao”

Baba, tunakiri kwamba wakati fulani hatutaki kusamehe. Tuweke huru kutoka katika uchungu na chuki. Badili mioyo yetu na uiruhusu neema

Yako itiririke kupitia kwetu hadi kwa wengine. Badilisha adui zetu kuwa marafiki na uunganishe mioyo yetu katika huduma kwa ajili ya ufalme Wako.

“Baba Yenu wa Mbinguni Atawasamehe Ninyi”

Asante Bwana, kwa zawadi tusizostahili za toba na ukombozi. Wakati mwingine tunahangaika kukubali msamaha Wako na kujaribu kupata kibali Chako. Tunaomba utufundishe kupokea msamaha Wako kwa furaha na kuieneza neema hiyo kwa wengine.

Mapendekezo ya Maombi Zaidi

Shukrani na Sifa: Shukuruni kwa baraka mahususi na Msifuni Mungu kwa wema Wake.

Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na umshukuru Mungu kwa msamaha Wake.

Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.

Kanisa Letu: Ombea mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).

Mahitaji ya Eneo Mahalia: Ombea mahitaji ya sasa ya washiriki wa kanisa, familia na majirani.

Sikiliza na Uitike: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa na nyimbo.

Mapendekezo ya Nyimbo

  • Nimekombolewa na Yesu (Vk. 178 & Vd. 35)
  • Yesu Mwokozi (Vk. 248 & Vd. 51)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *