Kutoka Kwa mchungaji wa mtaa Pr. Adam Gerold Simba


Wapendwa katika KRISTO habari. Awali ya mambo yote nitumie nafasi hii kuwashukuru sana sana kwa Moyo wenu wa kujali na kuthamini kwenu kazi ya BWANA. Nina washukuru sana kwa maombi yenu mnayoendelea kutuombea. Safari yetu yulisagiri salama na tumefika salama. BWANA amekuwa mwema. Asanteni sana kwa maombi yenu.

Ninawashukuru sana kwa ushirikiano mnao endelea kuwapatia Wazee wa Kanisa na Mzee/Mchungaji anayesimamia majukumu ya kichungaji kwa sasa Mzee Gibson Johnson Kisaka BWANA awabariki sana. Asanteni sana kwa kuwapatia ushirikiano katika majukumu ya kiutume BWANA awabariki sana.
Ninawaomba tuendelee kuombeana.

Aidha kwa niaba ya Uongozi wa Kanisa,nitumie wasaa huu kuwaalima na kuwaalika kila mmoja wenu kuhudhuria juma la maombi kwa kipindi chote cha siku 10 za Maombi zinazo anza tarehe 08 – 18/12/2025 amba zitaanza rasmi jumatano ya wiki hii (kesho kutwa). Ninawaomba kila mmoja wetu apange namna ya kushiriki mibaraka hiyo ya kuwa miguuni pa KRISTO pamoja na familia zetu. Natambua kuwa tunayo majukumu ya kikazi,kifamilia,Kanisa na kijamii pia,lakini tusiache kupanga kuwa na muda na BWANA hata kwa masaa hayo tu ya kuzungumza na BWANA kila jioni.

Mambo ya kuzingatia ni pamoja na;
(1) Andaa jirani zako,ndugu katika familia,na majina Yale ya wale tunao endelea kuwaombea kila siku (watu 10). Waalike kushiriki katika siku 10 hizi za Maombi.

(2) Ni jambo gani unalofikori umwambie BWANA katika siku 10 hizi za Maombi? Lipeleke kwa KRISTO yupo tayari kutusikia na yupo tayari kubeba mizigo yetu yote hebu tumtike yeye fadhaa zetu zote. Nawasihi sana kwa huruma zake BWANA usikose kuwa na muda na BWANA katika siku 10 hizi za Maombi. BWANA yupo tayari sasa kuturahisishia yale yote magumu tusiyo yaweza. Kusudia kushiki Baraka hizi.

(3) Kumbuka kuombea Kanisa katika ujumla wake;

(1) Tmwombe BWANA atupatie Roho wake Mtakatifu mara dufu. Ili tutende kazi kwa msukumo wa kuongozwa na Roho wake Mtakatifu.

(2) Ombea Viongozi wa Kanisa kuanzia ngazi za juu hadi Kanisa Mahalia.

(3) Ombea umoja wa Kanisa katika kipindi hiki cha siku za mwisho.

(4) Ombea uchaguzi wa Kanisa utakao anza ngazi za juu GC, DIVISION,UNION, KONFERENSI na Kanisa Mahalia MANZESE ili BWANA awatayarishe watu walio na Roho wa BWANA ndani yao watakao pokea kijiti cha kazi ya BWANA kutoka Watumishi wa BWANA wanaoendelea na Utumishi huo sasa kwa Kanisa MANZESE.

(5) Ombea Familia. Kwa walio oa na kuolewa tuombe ndoa zetu. Kwa ambao hawajaoa na kuolewa wao waombe BWANA awapatie wenzi Bora nasi tuwaombee katika hilo.

Na yatakayo jiri katika masomo yote ya siku kumi.

Ama kwa hakika tukiziendea siku hizo kwa maombi ya Imani BWANA atajifunua mwenyewe na Yale yaliyo kuwa magumu atayarahosisha.

Mhudumu ambaye atakuja kwetu kwa Huduma ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ECT Mchungaji William Izungo. Usipange kukosa.

Hata kumpata kwake ni ushuhuda Mkuu. Nawashuhidia leo hivi ni BWANA aliye mruhusu kuja kwa kusudi lake kwetu sote” tuungane pamoja naye kwa mahidhirio na kualika wengine. Ataingia mapema sana. Usipange kukosa. Upatapo ujumbe huu mwalike na jirani yako na ndugu na jamaa wa karibu nawe. BWANA awabariki sana. AMINA 🙏🙏🙏

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *